Watu wapatao saba wameuwawa na wengine 17 kujeruhiwa leo katika shambulizi lililofanywa na mtu wa kujitoa muhanga katika eneo la Taji, kaskazini mwa mji mkuu wa Iraq, Baghdad. Haikubainika mara moja kama shambulizi hilo liliilenga kambi ya jeshi au lango la kuingilia kambi hiyo na idadi ya washambuliaji haikujulikana. Wakufunzi wa jeshi la Marekani wako Taji wakisaidia kutoa mafunzo kwa wanajeshi 1,600 wa Iraq katika mpango utakaodumu wiki sita unaonuiwa kuwaandaa kukabiliana na kundi kigaidi la Daesh. Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na shambulizi hilo, lakini mashambulizi ya aina hiyo yamekuwa yakifanywa na makundi ya Sunni yenye itikadi kali nchini Iraq, likiwemo kundi la Daesh.
22 Januari 2015 - 20:04
Msimbo wa Habari: 666511
Watu wapatao saba wameuwawa na wengine 17 kujeruhiwa leo katika shambulizi lililofanywa na mtu wa kujitoa muhanga katika eneo la Taji